UHUSIANO WA MBINU ZA KUFUNDISHA SARUFI NA UMILISI WA MAZUNGUMZO YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI ZA UMMA, KAUNTI NDOGO YA KISUMU MASHARIKI.
- Department of Educational Communication & Technology University of Nairobi.
- Abstract
- Keywords
- References
- Cite This Article as
- Corresponding Author
Lugha ya Kiswahili kina dhima kubwa ulimwenguni katika kukidhi mahitaji ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na kielimu. Nchini Kenya, Kiswahili ni lugha ya taifa na rasmi. Isitoshe, Kiswahili ni somo la lazima linalofundishwa na kutahiniwa katika viwango vya shule za msingi na sekondari. Msingi wa lugha hii ni sarufi ambayo hutawala stadi zote za lugha. Licha ya dhima ya sarufi katika kufanikisha mawasiliano tafiti nyingi zinaonyesha kuwa wanafunzi wengi hawawezi kujieleza kwa usahihi na kwa ufasaha hata baada ya kuhitimu masomo ya msingi. Hali hii ilimchochea mtafiti wa kazi hii kuchunguza uhusiano uliopo kati ya mbinu za kufundisha sarufi na umilisi wa mazungumzo ya wanafunzi.Utafiti huu ulidhamiria kutimiza lengo lifuatayo: Kuchunguza mbinu zinazotumiwa na walimu kufunza sarufi ya Kiswahili. Utafiti huu ulifanyika katika Kaunti ndogo ya Kisumu Mashariki. Utafiti huu uliongozwa na nadharia ya mfumo katika utaratibu wa ufunzaji na ujifunzaji wa lugha ya pili.Muundo wa kimaelezo ulitumika. Mtafiti alitumia uteuzi sampuli kinasibu kuteua shule katika viwango vya kitaifa, kaunti na kaunti ndogo.Uteuzi makusudi ulitumika kuteua darasa la saba na walimu wao. Sampuli lengwa ya wanafunzi iliteuliwa kinasibu.Data ilikusanywa kutumia hojaji, mahojiano na utaratibu wa utazamaji darasani ili kuimarisha uaminifu na uthabiti wa data.Data iliyokusanywa ilichanganuliwa kwa muundo wa kimaelezo,kithamani na kiidadi.Data hii iliwasilishwa kwa kutumia majedwali na grafu.Matokeo yalionyesha kuwa walimu wengi walitumia mbinu ya mhadhara katika kufundisha sarufi huku mbinu za kisasa zinazowashirikisha wanafunzi zaidi zikipuuzwa.Utafiti pia ulidhihirisha kuwa wanafunzi hawashirikishwi ipasavyo katika mazoezi yanayoweza kuimarisha umilisi wa sarufi na mazungumzo.Isitoshe,matumizi ya chaki na ubao ulitawala utaratibu wa kufundisha sarufi huku vifaa vingi vikikosa kutumika.Hatimaye utafiti huu ulibainisha kuwa kuna uhusiano kati ya mbinu za kufundisha sarufi na umilisi wa mazungumzo ya wanafunzi.Utafiti huu ulipendekeza kuwa kuwepo na mafunzo kwa walimu kuhusu mbinu,mazoezi na vifaa mwafaka katika ufundishaji wa sarufi ili kuimarisha umilisi wa lugha ya Kiswahili.
- Abigael W. M. (2000). Factors influencing the performance of Kiswahiliin KCPE in Dagoreti Division, NairobiProvince. Unpublished MED Thesis; KenyattaUniversity.
- Babusa H. (2010). Uchanganuzi linganuzi wa mielekeo ?na umilisi wa lugha ya Kiswahili wa wanafunzi katika mikoa ya Pwani na Nairobi nchini Kenya. Unpublished PHD. Thesis. KenyattaUniversity.
- Bwire A.M. na Vikiru L.I. (2008). Approaches to the Teaching of Grammar and Vocabulary in Groenewegen Bencharks for English language Education, Phoenix Publishers Ltd. Nairobi.
- Crystal D. (1997). The Cambridge Encyclopedia of Language. Cambridge: CambridgeUniversity Press.
- Chimerah R. (1995). Kiswahili past present and Future Horizons.NairobiUniversity Press.
- Chiragdin, S. na Mnyampala (1977). Historia ya Kiswahili: Oxford University Press.
- Ellis, R. (1994). The study of second language Acquisition. London: OxfordUniversity Press.
- Gathumbi A. na Masembe, S. (2005). Principles and Techniques in Language Teaching. Nairobi. Jomo Kenyatta Foundation.
- Larnisen, F. D. (2003). Teaching language: From grammar to grammaring. Boston: Heinle and Heinle.
- Littlewood, W. (1981). Communicative Language Teaching ? An introduction. Cambridge: CambridgeUniversity Press.
- Mbaabu, I. na Nzunga M. (2008). Sheng? its major characteristics and impact in standard Kiswahili and English. Dar es salaam.
- Mbaabu, I. (1985). Sarufi ya Kiswahili. Nairobi: Kenya publishing and Book Marketing Company Ltd.
- Mbaabu, I. (1995). Usahihishaji ?wa makosa katika Kiswahili. Nairobi: Longman Kenya Ltd.
- Mckay S. (1985). Teaching Grammar: Form 1 Function and Techniques. New York: Pergamon Press
- Mgullu, R. S. (1999). Mtaala wa ?Isimu: Fonetiki, Fonolojia na Mofolojia ya Kiswahili. Longhorn Publishers, Nairobi.
- Momanyi, C. (2007). ?Nafasi ya Kiswahili katika Elimu ya vyuo vikuu nchini Kenya? katika Kiswahili na Elimu Nchini Kenya. Kolbe Press.
- Mugenda, O.M. na Mugenda A.G. (1999). Research Methods. Quantitative and Qualitative Approaches. Nairobi: Acts Press.
- Mwihaki, A.N. (2006). ?Sheng? ??na?? ?usomi wa Kiswahili, mtazamo wa kiisimu na Jamii. Makala ya semina ya Isimu jamii ambayo ilitolewa mjini Nakuru. Haijachapishwa.
- Orodho, J.A. (2003). Teachniques of Writing Research Proposal and Reports in Education and Social Sciences. (2nd) Kanezja HP. Enterprises, Nairobi.
- Republic of Kenya (1964). Kenya Education Commisssion Report (The Ominde Report). Nairobi: Government Printer.
- Republic of Kenya (1976). Report of the National committee of Educational policies and objectives (Gachathi Report), Nairobi: Government Printer.
- Kombo, D.K. na Tromp, D.L.A. (2006). Proposal and Thesis Writing: Nairobi: Paulines Publications Africa.
- Williams J. (2005). Form-focused instruction. In E. Hinkel (Ed). Handbook of research in second language teaching and learning. Mahwah. NJ: Lawrence Erlbaum Associates.
[Hellen Wambui. (2017); UHUSIANO WA MBINU ZA KUFUNDISHA SARUFI NA UMILISI WA MAZUNGUMZO YA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI ZA UMMA, KAUNTI NDOGO YA KISUMU MASHARIKI. Int. J. of Adv. Res. 5 (Nov). 34-40] (ISSN 2320-5407). www.journalijar.com
Department of Educational Communication & Technology University of Nairobi